Wazee kutoka wadi ya Isukha Magharibi eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega wamejitokeza kupinga pendekezo la baadhi ya wakazi kumtaka mwakilishi wadi wao Edward Shibembe kuwania kiti cha ubunge na badala yake wanamtaka kusalia kwenye kiti cha mwakilishi wadi
Wakiongozwa na Julius Likare wanamtaka Shibembe kukamilisha mipangilio yake kabla ya kusonga mbele kisiasa Kwa upande wake Edward Shibembe ambaye alitembelewa na waze hao nyumbani kwake eneo la Musingu amekubaliana na mapendekezo yao
