Kama moja wapo ya kujipanga kukabiliana na msambao na mkurupuko wa magonjwa mbalimbali sasa waziri wa afya kaunti ya Bungoma Antony Walela ameombwa kuzihami hospitali na zahanati zote katika kaunti ya Bungoma na vitanda vya kutosha.
Akizungumza ofisini mwake askofu mkuu kanisa la ki anglikana Philip Mechumo ametiilia shaka utepetevu ulioko katika wizara ya afya huku akisema kuwa ipo haja ya sekta hiyo muhimu kufanyia marekebisho miundo misingi na vifaa ili kuwafikia hata watu wengi zaidi.
Kuhusu malumbano ya mara kwa mara ya wanasiasa katika kaunti ya Bungoma askofu Mechumo amewataka vigogo wa kisiasa ukanda huu kuweka vichwa pamoja kama wana nia ya kuunda serikali mwaka wa 2022.
Askofu Mechumo aidha ametumia fursa hiyo kuwarai wakristo kote nchini kuiombea nchi haswaa msimu huu dunia inapopitia changamoto za kiuchumi kufuatia changa kuu la korona.
By Hillary Karungani