Idara ya utawala eneo bunge la Shinyalu  kaunti ya Kakamega yatoa tahadhari kwa wamiliki wa maduka ya kuuza nyama kuwauzia wateja nyama kutoka kwa mifugo zilizofariki huku pia madaktari wa mifugo wakilaumiwa pakubwa kwa kushirikiana na wahusika kwa kutia alama ya mihuri kwa hizo.

Haya ni kwa mujibu wa chifu wa kata ya Khayega eneo bunge hilo Gerald Murunga na mwenyekiti wa nyumba kumi Muhanji Alusa, wanaosema wengi wa wananchi wanakabiliwa magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na nyama isiyodhibitiwa kwa utumizi na madaktari wa mifugo.

wamefichua kuwa wengi wa madaktari wa mifugo wanashirikiana na wezi wa mifugo ambao wanaiba mifugo na kisha kuzichinja ndani ya misitu na nyumba kabla ya kuzipeleka kwenye maduka ya kuuza nyuma.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE