Pendekezo la waziri wa elimu, prof. George Magoha kua kuna mpango wa kuondoa shule za bweni linazidi kupokea hisia mseto ikizingatiwa kua waziri hakutoa sababu za kuafiki wazo hilo. Wengi wa washikadau wa elimu wanapinga pendekezo hilo wakisema kua waziri hakuwausisha katika kufikia uamuzi. Katika mahojiano ya moja kwa moja na kituo hiki, mwalimu mkuu wa shule ya upili ya ebambwa, jeremiah andayi alisema kua pendekezo la waziri linahitaji muda wa kushaurina.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Kyakatoni ilioko kaunti ya Makueni, Paul Meja ambaye alikua katika likizo mjini Kakamega alisema kua pendekezo la waziri litahujumu mpango wa wizara wa kuwatawanya walimu kutoka sehemu walizozaliwa.


Wakuu hao wa shule walilalamikia majengo machache ya shule ya upili ya Ebambwa ikizingatiwa kua idadi ya wanafunzi imeongezeka pakubwa. Walitoa wito kwa wahisani kuingilia kati ili kuwawezesha kusajili wanafunzi zaidi.

By Wycliffe Andabwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE