0202322172

info@lubaofm.co.ke

Uniting Communities

Listen Live

102.2 FM Live

ON AIR

UP NEXT

Liverpool imejitokeza kumsaka mshambuliaji wa Poland

Liverpool imejitokeza kama mojawapo ya klabu ambazo zinamsaka mshambuliaji wa Poland na Bayern Munich Robert Lewandowski wa miaka 33, ambaye anatarajiwa kuondoka katika Bayern Munich msimu ujao

Hayo  yakijiri Manchester United wamekuwa na mazungumzo mazuri na kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes tangu mwezi julai. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anataka kusalia Old Trafford na kandarasi yake inachukuliwa na umuhimu mkubwa pamoja na kiungo wa kati paul pogba, 28

Kadhalika United ilitaka kufanya mazungumzo ya makubaliano na Napoli ili kumsajili nahodha wa Senegal Kalidou Koulibaly, 30, msimu ujao lakini hawakuwa tayari kukubali thamani ya mchezaji huyo kama inavyodaiwa na klabu hiyo ya serie a ya £34m kumnunua beki huyo wa kati.

Na Beki wa Chelsea Antonio Rudiger huenda akauzwa ili kufadhili ununuzi wa beki wa Sevilla Jules Kounde . Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Ujerumani ananyatiwa na klabu za PSG na Real Madrid , lakini ameonekana kuwa kiungo muhimu wa safu ya ulinzi wa mkufunzi Thomas Tuchel

By Samson Nyongesa

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

RSS
Follow by Email