Mbunge wa Sirisia John Koyi Waluke amewataka wakaazi wa eneo hilo kukumbatia kilimo cha pamba akidokeza kuwa tayari serikali iko katika harakati za kukifufua kiwanda cha kutengeneza pamba mjini malakisi.
Akihutubu kwenye hafla ya mazishi eneo la Bisunu eneobunge la Sirisia Waluke amehoji kuwa hivi karibuni kiwanda cha kutengeneza pamba mjini malakisi kitaanza kufanya kazi na kuwataka wakaazi hao kukumbatia kilimo hicho akisema kitawawezesha kujikimu ikilinganishwa na kilimo cha tobako ambacho malipo yake ni duni.
Aidha waluke amewataka wazazi kuwapeleka wanao shuleni akidokeza kuwahivi karibuni hazina ya CDF eneo hilo itaanza mchujo wa kuwapa basari watoto werevu, kutoka jamii maskini huku akiwaonya wanaume dhidi ya kushiriki tendo la ngono na watoto wa shule.
Amewataka wananchi kuwaheshimu viongozi wote waliochaguliwa na kufanya uamuzi wa busara hasa kwenye uchaguzi mdogo wa Kabuchai na uchaguzi mkuu ujao.
Story By Richard Milimu