Kulizuka kizaazaa katika afisi za benki ya KCB mjini Kakamega mapema hii leo baada ya wazee na wazazi wa watoto walio na changamoto za ulemavu kulalamikia kusumbuliwa na usimamizi wa benki hiyo.


Wakizungumza nje ya benki hiyo wananchi hao wamesema kuwa wanapitia wakati mgumu wa kifedha huku benki hiyo ambayo imepewa jukumu la kuwalipa wazee hao pesa za usaidizi wa kila mwezi kutoka kwa serikali kuu ikiwazungusha huku na kule.

Wameitaka serikali kuu kupitia afisi husika kuwabadilisha kutoka kwenye benki hiyo na kuwasajili katika benki ambayo hawatapata shida kupokea senti zao za kila mwezi , wakidai kuwa usimamizi wa benki ya KCB sekta ya malipo yao unautepetevu.


Kulingana na wazee hawa wamemaliza zaidi ya miezi mitatu bila kulipwa pesa zao.

Juhudi za kupata maoni ya usimamizi wa benki hii hazikufanikiwa baada ya meneja kudinda kuongea na wanahabari afisini mwake.

 By Kefa Linda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE