Wafanya biashara wa minada hasa wa kununua mifugo walalamikia kupanda
Kwa bei wa mifugo kama vile, mbuzi, kondoo na ngombe sokoni ikilinganishwa na
Hapo awali.kwa sasa inawalazimu wao kutembea kilomitre nyingi kwa shughuli
Ya kutafuta wateja wao ambao mara nyingi huenda wakakosekana.ingawa kwa
Wengine hupata manufaa wengi wao hubaki kuifanya tu kama kazi ya bora
Mkono kinywani.
Bei ya ng’ombe iko juu sana sasa hatuna wateja wa kununua ng’ombe sasa sijui tunafanyaje kwasababu wateja wetu wengi ni wa kuchija
Kwa huo ukosefu wa kuuza wengi wao hubidi kutumia mbinu mbadala za kupata
Fedha kupitia kazi hii aghalabu kwa kuukopesha wanaochinja vichinjioni au kuuza
Kwa bei duni ambayo huwa ni hasara.
Lakini hii biashara lazima uwe na mtu wa kichinjio ambaye atakua anachukua hiyo mifugo. Kwa sasa inabidi tukopeshe kwa sababu uwezi rudi nazo nyumbani na ng’ombe huwa pia inachoka na ukishakopesha mteja ataa kulipa polepole.
By Austine Shambetsa