Mwanafunzi wa kidato cha tatu azuiliwa kwenye kituo cha polisi baada ya kumshambulia babake katika kijiji cha Barotion eneo la Londiani kaunti ya Kericho
akithibitisha kisa, hicho chifu wa eneo hilo Sarah Sigey alisema kwamba mzozo ulikuwa baina yao baada ya mshikiwa huyo kufika nyumbani na kupata baba akiwa ameuza kuku iliyokuwa yake bila kumuliza


Kijana huyo inasemekana kuwa aligombana na baba yake ambaye alimkataza.Mshukiwa alichukua fimbo na kumgonga baba yake mara kadha wa kadha
majirani walikimbia kwa boma hilo na kumuokoa mzee huyo mwenye miaka hamsini na kumukimbiza hospitali ya Londiani ambapo aliaga dunia akiwa kwenye matibabu


Baada ya kutekeleza mauwaji yale mwanafunzi huyu alijipeleka kwenye kituo cha polisi cha Londiani ambapo anazuiliwa huku akingojea kupelekwa mahakamani
mwili wa mwendazake ulitolewa na kupelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha St Joseph  eneo la Molo huku uchukuzi ukiendelea
BY BRIAN KINYANJI

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE