Siku moja baada ya wanachama wa UDA kukamatwa kwa madai ya kununua vitambulisho kwa wakazi, sasa mwakilishi wa wadi ya Shirere mwalimu David Ikunza anataka uchunguzi wa kina kufanywa na hatua kuchukuliwa
Licha ya wasimamizi wa chama cha UDA kukanusha madai hayo, Ikunza amesema vitendo sawia na hiki huenda vinalenga kusambaratisha Kura ya jamii ya waluhya
Wakati uo huo Ikunza anaitaka serikali kufanya uchunguzi na kurekebisha swala la wakenya kujipata wamesajiliwa kwa vyama vya kisiasa bila idhini yao
By Linda Adhiambo