Viongozi wa chama Cha ODM katika Kaunti ya Kakamega wamewasuta vikali wale wanaopanga njama ya kuzua rabsha katika ziara ya Rais Uhuru Kenyatta mwishoni mwa wiki kuwa katu hawatafaulu kwani Rais ako huru kuzuru kokote na kwamba kama chama watahakikisha ziara hiyo itafana kwa manufaa ya wakazi wa Magharibi ya Kenya.

Kwenye mkao na waandishi wa habari, mjini Kakamega, chama Cha ODM kupitia mbunge wa Shinyalu, Justus Kizito, viongozi hao wameeleza bayana kuwa baadhi ya vyama vinavyojipiga kifua kuwa na ufuasi mkubwa katika eneo la Magharibi na kula njama ya kuvuruga ziara ya Rais Kenyatta kamwe hawatafaulu kwani watafanya kila wawezalo kuhakikidha ziara hiyo inafanikiwa na kufaidi eneo zima la Magharibi ya Kenya.

Wanachama wa ODM wanashikilia kuwa hakuna sababu ya chama Cha ANC kushinikiza kujumuishwa katika ziara ya Rais Kenyatta kikamilifu kwa ni Gavana Wycliffe Oparanya na Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa waliotwikwa jukumu na kusukumu gurudumu la maendeleo katika eneo la Magharibi hivyo watakuwa wakitekeleza wajibu wao wa kumueleza Rais Kenyatta hatua walizopiga hadi sasa.

By Lindah Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE