Zaidi ya wanafunzi elfu tano werevu kutoka jamii zisizojiweza kutoka eneobunge la Kabuchai kaunti ya Bungoma wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza wamenufaika na ufadhili wa basari ya shilingi milioni kumi na nane kutoka afisi ya hazina ya CDF ya eneo hilo.

Akihutubu kwenye hafla ya kuzindua rasmi ugavi wa basari hizo katika afisi za hazina ya CDF eneo la Musese, mbunge wa Kabuchai Majimbo Kalasinga amedokeza kuwa wanafunzi elfu tano wamenufaika na ufadhili huo huku akiwatahadharisha dhidi ya kujiingiza katika visa vya utovu wa nidhamu shuleni.

Wakati uo huo Majimbo amekitaka chama cha ODM kuwasilisha mgao wa fedha ambao Ford Kenya inakidai hasa baada ya Ford Kenya hapo jana kutangaza rasmi kujiondoa kwenye muungano wa kisiasa wa nasa  baada ya mkutano wa kitaifa wa wanachama kuandaliwa jijini nairobi na kuhoji kuwa seneta wa kaunti hii Moses Wetangula alitwikwa jana jukumu la kutafuta urafiki na vyama vingine.

Kwa upande wake kiongozi wa wasanii kaunti ya Bungoma, Kasembeli Watila akikashifu kisa cha hapo juzi ambapo mbunge wa Kimilili Didmus Barasa alionekana akimzaba kofi mwanakadarasi Stephen Masinde almaarufu Steve Kay, na kudokeza kuwa kama wasanii watashiriki maandamano ya amani kulalamikia kisa hicho.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE