Huku waumini wa kanisa  la kikatoliki wakiendelea kuomboleza  Fr Christopher Wanyonyi aliyekuwa akisimamia kanisa la Kathedrali la Christ The King Bungoma  wa hivi punde kumminia sifa ni mjumbe wa Kanduyi Atanasi Wafula Wamunyinyi.

Kwenye ujumbe wake kwa wanahabari Wamunyinyi amemtaja  Fr Wanyonyi  kama kiongizi jasiri wa kiroho ambaye  alijitolea kubadilisha maisha ya wengi sio kupitia kwa mahubiri tu bali pia kupitia kwa misaada ya moja kwa moja.

Mjumbe huyo aidha amesema kuwa atamkumbuka zaidi Fr Wanyonyi katika juhudi zake za kuwapatanisha viongozi wa kisiasa kaunti ya Bungoma na ukanda huu wa  Magharibi  kwa ujumla huku akisema kuwa pengo aliloliacha Fr Wanyonyi litakuwa ngumu kuzibika.

Wakati uo huo mjumbe huyo ametumia fursa hiyo kutoa risala za rambi rambi kwa jamii ya mwenda zake Fr Wanyonyi na jamii pana ya kanisa la kikatoliki kwa kumpoteza kiongozi shupavu na mjapa kazi huku akiwahakikishia kuwa pamoja nao haswaa msimu huu wa majonzi..

Mwenda zake Fr Wanyonyi alitupa mkono wa buriani usiku wa kuamkia jumatatu wiki hii katika hospitali ya Rufaa Eldoret  akiwa kwenye mashine ya ICU akiyapokea matibabu.

Fr Wanyonyi ameishi duniani takribani miaka 63 huku akikumbukwa sana  kwa kujenga Kathedaral ambaye ni miongoni mwa Kadhedrali  kubwa nchini iliyo karimu takribani shilingi millioni mia moja.

Fr Wanyonyi anatarajiwa kuzikwa katika makaazi takatifu ya wafu katika  eneo ya kibabii  eneo bunge ya kanduyi, kaunti ya bungoma

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Mungu ailaze roho yake mahala pema Mbinguni

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE