Hisia mseto zimeibuka kuhusu hatua ya tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kuweka kiwango cha fedha kinachostahili kutumika na wagombeaji wa nyadhifa mbalimbali za kisiasa huku mbunge wa Teso Kusini Geofrey Omuse akidai kuwa itachochea ufisadi.

Akiongea katika eneo la Chakol na Kotur eneo bunge la Teso Kusini kwenye ufunguzi wa afisi ya tarafa ya Chakol, afisi ya chifu na kambi ya polisi mtawalia, Omuse amesisitiza kuwa wagombeaji wanastahili kutumia fedha kuambatana na uwezo wao mbali na kushawishi wapiga kura.

Kando na hayo Omuse ameshutumu vikali hatua ya  jaji mkuu wa zamani David Maraga kutaka uchaguzi mkuu wa 2022 kuhairishwa, akimtaka kujitenga na maswala ya siasa.

Omuse aidha ameelezea mikakati aliyonayo katika kuimarisha usalama ikiwa ni pamoja na kujenga afisi zaidi ya watawala kwa lengo la kuleta hudma karibu na wananchi.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE