Mamia ya vijana kutoka kaunti ndogo ya Cheptais eneo bunge la Mlima Elgon  wamejitokeza kushiriki mahojiano ya kuwatafuta wasimamizi wa vijiji (Village Administrator) kwenye ukumbi wa afisi  za naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Cheptais.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo mjini Cheptais eneo bunge la Mlima Elgon, mwenyekiti wa bodi ya kuwaajiri wafanyikazi wa umma kaunti ya Bungoma Jonathan Namulala, amesema zoezi hilo limeendeshwa kwa njia huru na haki huku akidokeza kuwa bodi hiyo inapania kutamatisha shughuli hiyo mapema mwezi ujao.

Wakati uo huo Namulala amepuzilia mbali madai kuwa tayari kuna vijana ambao tayari wameteuliwa kuchukua nafasi hizo akisema madai hayo ni ya kupotosha na hayana msingi wowote.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE