Biwi la simanzi limetanda mtaa wa Nyayo Tea Zone wadi ya Makhialo viungani mwa mji wa Kakamega baada ya mwanafunzi mmoja wa miaka 11 kutumbukia ndani ya mto Isikhu alikokuwa akijaribu kuogela.

Ni kumbukumbu za Pamela Anota, mamake Trevan Indavale Ambako anasema mtoto wake mwanafunzi wa grade ya nne katika shule ya Shitaho Community alikuwa ameenda kwa matanga ya jamaa wao eneo hilo kabla ya kushawishiwa na wenzake kuenda kuogelea alikoskumwa ndani ya maji na kuzama.

Aidha wakaazi eneo hilo wakiongozwa na Diana Ayuma wamelalamika kuwapoteza jamaa zao mara kwa mara kila mto huo unapofurika huku wakiitaka serikali ya kaunti hiyo kuwaajiri kama wapiga mbizi watakaosaidia kwa shughuli za uokozi kwa kisingizio ya kuwa na uhafamu wa kutosha kuhusu mto huo.

Ni kisa kilichodhibitishwa na mzee wa mtaa hiyo Edgar Masengo aliyewataka wakaazi kuwa waangalifu haswa msimu huu wa mvua kubwa kuepuka ajali sawia na hiyo huku mwakilishi wadi wa eneo hilo David Shikala akiahidi kuwasilisha mswada bungeni ya kuitaka bunge la kaunti hiyo kutenga mgao mkubwa utakao saidia kwa mikasa kama hizo ili kuokoa maisha.

By Richard milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE